- 162 viewsDuration: 1:48Familia za watu wawili waliopigwa risasi wakati wa maandamano yaliyofanyika siku ya jumanne katika eneo la ishiara kaunti ya Embu kulalamikia hali mbaya ya hospitali inalilia haki . Familia hizo zizikijiandaa kwa mazishi, familia hizo zinataka maafisa wa usalama waliohusika wachukuliwe hatua za kisheria wakisema wana wao walikuwa wakidai haki kupitia maandamano ya kikatiba na hawakuwa na silaha zozote. mmoja wa waathiriwa aliuwawa kwa kupigwa risasi shingoni huku mwingine akipigwa risasi mdomoni mita 150 karibu na hospitali ya Ishiara. wakazi wanataka OCS wa kituo cha polisi cha ishiara ahamishwe.