- 100 viewsFamilia zinazoishi karibu na mto tana huko garissa zimeanza kuhama baada ya mto tana kuvunja kingo zake kutokana na kuongezeka kwa viwango vya maji. Familia hizo zinahangaika kwa kukosa mahala pa kwenda. Aidha wanahofia kukosa chakula kwani sasa wamejihifadhi kwenye kambi za muda.