Skip to main content
Skip to main content

FKF yaanza kusaka vipaji kuunda Machakos All Stars

  • | Citizen TV
    36 views
    Tawi la FKF kaunti ya Machakos limeanzisha mpango wa utafutaji wa vipaji ili kuunda timu ya Machakos All Stars FC kwa wanaume na wanawake. Zoezi hilo la kutafuta vipaji limeanza katika kaunti ndogo ya masinga ambapo wachezaji 30 walichaguliwa kuiwakilisha masinga All Stars huku zoezi hilo likielekea katika kaunti ndogo za Yatta, Mwala, Kangundo, Kathiani, Machakos, Mavoko, Matungulu na Kalama. Aliyekuwa nahodha wa Harambee Stars Musa Otieno aliongoza wakufunzi kutambua vipaji.