- 7,649 viewsDuration: 3:09Kinara wa DCP Rigathi Gachagua sasa anadai kuwa wahuni wanaovamia mikutano ya upinzani ni maafisa wa polisi wanaovaa mavazi ya kihuni ili kuchora picha kuwa upinzani umejaa vurugu. Akiibua madai hayo alipozuru Murang’a Jumanne, Gachagua ameendelea kudai kuwa wahuni hao wanapata maelekezo kutoka serikalini akisisitiza kuwa hawatakoma kuikosoa serikali hata kwa vitisho. Na kama anavyoarifu Kamau Mwangi, usemi wa Gachagua umerejelewa na kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka aliyefanya kikao na wagombea wa chama hicho huko Taita Taveta.