Serikali ya Kaunti ya Machakos imezindua ujenzi wa hospitali ya rufaa na mafunzo ili kuhakikisha wakazi wanapata matibabu ya kisasa.
Hospitali hiyo ya Muindi Mbingu inayojengwa kupitia ushirikiano na sekta ya kibinafsi, inatazamiwa kupunguza msongamano katika hospitali zingine za kaunti hiyo.Gavana wa Machakos Wavinya Ndeti alizindua vifaa kwa hospitali za Matuu, Mwala, Kangundo, na Machakos Level 5, hii ikiwa ni awamu ya kwanza ya mpango mpana wa kuimarisha uwezo wa hospitali hizo kutoa huduma za uchunguzi na kimatibabu.