- 429 viewsDuration: 2:07Kamati ya Seneti kuhusu Afya imebaini hali mbaya ya huduma za afya katika Kaunti ya Baringo baada ya ziara ya ukaguzi iliyoongozwa na Mwenyekiti wake, Jackson Mandago. Ziara hiyo iligeuka kuwa tathmini ya dharura baada ya kamati kupata miundombinu chakavu, uhaba wa dawa, na vifaa tiba visivyofanya kazi katika hospitali kadhaa za kaunti hiyo.