Skip to main content
Skip to main content

Hasira ya risasi yazua maandamano baada ya kijana kupigwa risasi nyumbani

  • | Citizen TV
    9,171 views
    Duration: 3:10
    Wakazi mtaani Huruma hapa Nairobi waliandamana leo kulalamikia kupigwa risasi kwa mvulana wa miaka 14 hapo jana. Wakazi hao wanasema wanaume wanne waliovalia kiraia na kujitambulisha kuwa maafisa wa polisi walitofautiana na wakazi wakati wa uchunguzi wa kisa cha uhalifu na kudaiwa kufyatua risasi hewani ili kutawanya wakazi. mtoto huyu akiripotiwa kupigwa risasi akiwa kwenye roshani ya nyumba yao.