Skip to main content
Skip to main content

Hazina ya kitaifa yapendekeza bajeti ya shilingi trilioni 4.8 kwa 2026/2027

  • | Citizen TV
    533 views
    Duration: 3:11
    Hazina ya Kitaifa inapendekeza bajeti ya shilingi trilioni 4.8 katika mwaka wa kifedha wa 2026/2027 utakaonza mwezi Julai mwaka huu. Kwenye makadirio ya bajeti yaliyowasilishwa bungeni, Hazina ya Kitaifa inapendekeza kuongeza mgao wa serikali za kaunti kwa shilingi bilioni tano, hali ambayo itafanya mgao huo kuwa na shilingi bilioni 420. Ili kufadhili bajeti hii, serikali inanuiwa kukopa zaidi ya shilingi trilioni 1.1, ambapo mkopo mkubwa utatoka kwenye benki za humu nchini.