Skip to main content
Skip to main content

Huzuni makafani Naivasha wazazi wakitambua miili ya wanafunzi waliofariki moto Gilgil

  • | Citizen TV
    1,128 views
    Huzuni, uchungu na majonzi zilihanikiza katika makafani ya hospitali ya Naivasha pale wazazi wa wanafunzi 16 waliofariki kwenye mkasa wa moto katika shule ya wasichana ya Utumishi walifika kutambua miili ya wana wao. Machozi yaliwatiririka kwa uchungu huku wakiangua vilio vya maumivu walipokuwa wakitazama miili ya wana wao kwa mara ya kwanza tangu mkasa huo kutokea siku ya Alhamisi. Baadhi yao walitaka kuchukua miili ya wana wao kwa mazishi ila walitakiwa kusubiri hadi uchunguzi wa DNA ukamilike