- 2,324 viewsDuration: 1:19Ida Odinga, balozi wa Kenya na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu mazingira, sasa anasema amechukua muda kumuomboleza mumewe, waziri wa zamani Raila Odinga, na hivyo kujitenga kwenye siasa. Akizungumza mjini Mombasa, Ida amesema kuwa yeye si mwanasiasa na hatajihusisha na siasa zinazoendelea. Amesema kuna wengine kwenye familia yake ambao wanahusika na masuala ya kisiasa.