- 244 viewsDuration: 1:51Tume ya uhaguzi na mipaka IEBC imewataka wananchi kujitokeza na kujisajili kama wapiga kura ili kuweza kuwachagua viongozi waadilifu. Wakizungumza katika hafla ya kutoa hamasisho kwa umma Kuhusu masuala ya uongozi, wadau hao wamesema wameweka mikakati ya kuwafikia wapiga kura ili kuhakikisha wanaelewa umuhimu wa kuwachagua viongozi wanaostahili. Aidha viongozi wa kisiasa na wa kidini wametakiwa kuwa mstari wa mbele kuhamasisha umma kuhusu umuhimu wa kufanya maamuzi ya uongozi kwa kujisajili na kupiga kura ili kufanikisha maendeleo.