- 496 viewsDuration: 2:40Tume ya Uchaguzi IEBC imetangaza kwamba itaongeza idadi ya nchi ambazo Wakenya wanaweza kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka ujao kutoka 12 hadi 26. Akizungumza mbele ya Kamati ya Bunge ya maswala ya kigeni, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa IEBC Ledama Sunkuli aliomba Bunge kuongeza bajeti ya tume hiyo, akisema walikuwa wameomba shilingi milioni 500 lakini wakapewa milioni 400 pekee. tume hiyo bado haijaanza elimu na usajili wa wapiga kura walioko ughaibuni kutokana na upungufu wa fedha.