IPOA yaanzisha uchunguzi wa mauaji ya mwanablogu Albert Ojwang, Central Police

  • | Citizen TV
    258 views

    Inspekta Jenerali wa polisi Douglas Kanja amefichua kuwa naibu wake, Eliud Kipkoech Lagat ndiye mlalamishi aliyesababisha kukamatwa kwa mwanablogu Albert Ojwang'. Kanja amesema kuwa Lagat aliwasilisha malalamishi ya kuharibiwa jina na Ojwang', ambaye alipatikana amepoteza fahamu katika njia tatanishi katika kituo cha polisi cha central hapa jijini nairobi na kisha kufariki akipelekwa katika hospitali ya Mbagathi.Kanja pia amesema kuwa maafisa wote wa polisi waliokuwa kazini katika kituo hicho wamesimamishwa kazi huku ipoa ikianzisha uchunguzi.