Skip to main content
Skip to main content

Jeshi la ulinzi laadhimisha siku ya Ushirikiano

  • | KBC Video
    165 views
    Duration: 3:46
    Serikali imeweka mikakati mbalimbali kushughulikia changamoto zinazoibuka na za kiusalama humu nchini na nje ya mipaka yake. Akizungumza wakati wa sherehe ya 14 ya siku ya Ushirikiano ya Jeshi la Ulinzi la Kenya iliyoandaliwa katika uwanja wa michezo wa Ulinzi, jijini Nairobi, naibu mkuu wa jeshi la ulinzi, jenertali mstaafu John Omenda, alisema kuwa Kenya pamoja na maeneo mengine duniani bado inakabiliwa na vitisho vinavyoongezeka na vinavyohusiana, ukiwemo ugaidi,itikadi kali na uharamia. Aidha, alitaka nchi wanachama, hasa za Jumuiya ya Afrika Mashariki, kuungana ili kukabiliana na changamoto hizo za kiusalama. Mwanahabari wetu Timothy Kipnusu ametuandalia taarifa hiyo. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive