"Jirani zetu wa Tanzania kama tumewakosea tunaomba radhi"

  • | BBC Swahili
    29,603 views
    Rais wa Kenya William Ruto Rais William Ruto ameomba radhi mataifa jirani ya Uganda na Tanzania katika hatua ambayo inaonekana kama juhudi za kuimarisha uhusiano kati ya mataifa hayo ya Afrika Mashariki. Akizungumza wakati wa dhifa ya maombi ya Kitaifa jijini Nairobi, Rais Ruto alitoa wito wa kuboreshwa kwa uhusiano, akibainisha kuwa Kenya ipo katikaharakati ya "kujijenga upya". Kauli ya Ruto inakuja wakati ambapo mvutano umeibuka kufuatia hatua ya Tanzania kuwatimua wanaharakati wa Kenya waliokuwa wamesafari hadi nchini humo kushuhudia kusikilizwa kwa kesi kiongozi wa upinzani Tundu Lissu. #bbcswahili #kenya #tanzania Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw