- 154 viewsDuration: 2:02Kamati ya usalama ya kaunti ndogo za Bangale na Tana Kaskazini imefanya kikao na wazee wa jamii mbili zinazozozania lsehemu za malisho na maji ili kuweka kanuni mpya za kuzuia uhasama. Kati ya kanuni hizo ni kuwa kila jamii ni sharti ihusishe maafisa wa usalama wakati wa kusaka mifugo wanaodhaniwa kupotea na vile vile kuandaa mikutano ya amani katika kila kijiji ili kuleta jamii hizo pamoja. Aidha wanajamii wametakiwa kurejesha silaha haramu wanazomiliki kinyume cha sheria ili kufanikisha juhudi za amani eneo hilo.