Kampuni za kutengeza vileo zapewa leseni upya

  • | Citizen TV
    316 views

    Naibu Rais Rigathi Gachagua amewaonya maafisa wa usalama na machifu dhidi ya kujihusisha na ufisadi unaochangia kuenea kwa utumizi na uuzaji wa pombe haramu nchini. Gachagua amesema kuwa serikali haitawasaza wasimamizi wanaovuruga mikakati ya kukabiliana na utumizi wa pombe haramu na hata mihadarati. Akizungumza wakati wa mkutano kuhusu pombe haramu kaunti ya Tharaka Nithi, Gachagua pamoja na waziri wa usalama wa kitaifa Profesa Kithure Kindiki wamesema kuwa serikali itatoa upya leseni za watengenezaji vileo ili kuwanasa wanaotumia leseni zao kutengeneza pombe ghushi. Waziri Kindiki hata hivyo amesema kuwa biashara zinazoendeshwa kwa njia iliyo halali zitalindwa