- 295 viewsDuration: 1:46Katibu katika wizara ya afya ya Umma Mary Muthoni ametahadharisha wasimamizi wa hospitali za ngazi ya pili dhidi ya kuhangaisha wagonjwa wanaotafuta huduma za matibabu kwa kutumia bima ya afya ya jamii SHA. Akizungumza katika chuo cha mafunzo cha udaktari ya Nyamache ( KMTC) kule Bobasi kaunti ya Kisii katika ziara maalum ya kukagua hali ya chuo hicho na changamoto zinazkikumba, Katibu huyo amesisitiza kuwa SHA inalipia gharama za vipimo vya wagonjwa na hivyo hawafai kutumwa nje na kurejea na matokeo hospitalini.