- 190 viewsDuration: 1:47Serikali ya kaunti ya Uasin Gishu kwa ushikiano na shirika moja lisilo la serikali imetia saini mkataba wa kuwasaidia vijana katika kaunti hiyo kuanzisha kilimo cha kisasa pamoja na kilimo biashara. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mjini Eldoret, Gavana Jonathan Bii amesema, kilimo ndio sekta ya pekee iliyo na nafasi nyingi za kazi kwa vijana na pia ina mapato makubwa. Shirika hilo la SNV linalenga vijana elfu 200 katika mpango huu kote nchini