Skip to main content
Skip to main content

Kinyang'anyiro cha Isiolo South

  • | Citizen TV
    188 views
    Duration: 48s
    Kinyang’anyiro cha kiti cha ubunge cha isiolo south sasa kimeng'oa nanga baada ya tume huru ya uchaguzi na mipaka -iebc - kuanza zoezi la kuwaidhinisha walioonyesha nia ya kuwania kiti hicho. Kinyang'anyiro hicho kimewavutia wagombea kadhaa wakiwemo mwanawe marehemu mohamed tubi wa uda, dadake mohammed bina tubi wa jubilee, pamoja na aliyekuwa mwakilishi wa wadi ya kinna, isaack fayo wa nedp. Isaack fayo anatarajiwa kuwasilisha stakabadhi zake za uteuzi kwa iebc baadaye leo.uchaguzi mdogo wa ubunge eneo hilo uliopangwa kufanyika tarehe 26 mwezi februari. Wakazi wanamchagua tena mbunge kufuatia kifo cha mohamed tubi bidu aliyeaga dunia novemba mwaka jana.