Viongozi katika kaunti ya Nyamira wametoa changamoto kwa wazazi, maafisa wa elimu na serikali kutia juhudi zaidi, kuhakikisha wanafunzi wa gredi ya kumi wanarejelea masomo.
Mwakilishi wa kike katika kaunti hiyo Jerusha Momanyi amehimiza jamii kutoa ripoti kuhusu wanafunzi ambao hajafanikiwa kwenda shuleni ili hatua mwafaka kuchukuliwa. Aidha Seneta wa Nyamira Okong'o Omogeni naye ameisuta serikali kwa madai ya utepetevu katika zoezi la kuwasaka wanafunzi ambao wangali nyumbani, akidai serikali imeshindwa na majukumu yake.