"Kuona picha za kaka yangu akiwa amekonda kama mifupa ni aina ya ukatili,"

  • | BBC Swahili
    622 views
    Hamas ilitoa video Jumamosi inayoonyesha Evyatar David, kaka wa Ilay mwenye umri wa miaka 24 akiwa ndani ya handaki akichimba kaburi ambalo anasema ni kwa ajili yake mwenyewe. Video hiyo, inayomwonyesha mateka huyo akiwa amedhoofika sana ndani ya handaki, imelaaniwa vikali na viongozi wa Israel na mataifa ya Magharibi. Kitengo cha kijeshi cha Hamas kimekanusha madai kwamba kinawalaza njaa mateka kwa makusudi, kikisema kuwa mateka hula kile wanachokula wapiganaji wao pamoja na raia wa Gaza. #bbcswahili #hamas #Israel Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw