KUPPET tawi la Samburu yataka Sekondari msingi kuendelezwa katika shule za upili

  • | Citizen TV
    160 views

    Chama cha kutetea maslahi ya walimu wa shule za sekondari na vyuo vya kadri KUPPET tawi la Samburu, kimetoa wito kwa Serikali kubatilisha uamuzi wa kuendeleza elimu ya sekondari msingi katika shule za msingi na badala yake kuendeleza elimu hiyo katika shule za sekondari. Kulingana nao, shule za upili zina mindombinu bora ya elimu ya sekondari zikilinganishwa na za msingi