- 597 viewsDuration: 1:41Muungano wa maafisa tabibu nchini wamepinga sera mpya zilizopendekezwa na serikali kuhusu sekta hiyo na kutishia kuelekea mahakamani iwapo itatekelezwa bila kuwahusisha kikamilifu. Wakizungumza mjini Mombasa, baada ya kuhudhuria kikao cha kukusanya maoni kuhusu sera hiyo muungano wa matabibu unadai mabadiliko hayo yamekuwa yakiendelea bila kupewa fursa ya kutoa mchango wao na hivyo kutaka zoezi hilo kusitishwa wakidai sera hiyo itakumbwa na masuala tata.