- 876 viewsDuration: 3:33Madereva wa masafa marefu wanaotumia barabara kuu ya Kisumu kwenda Busia na ile ya Eldoret kuelekea Malaba wanalalamikia kudorora kwa usalama katika barabara hizo, visa vya wizi vikikithiri wanaposubiri katika foleni kuvusha shehena zao mpakani. Wakizungumza kwenye foleni ya magari hayo katika mji wa mpakani wa Busia, madereva hao wameitaka serikali kutafuta suluhu ya kudumu kwa tatizo sugu la msongamano wa malori hayo katika mpaka wa Kenya na Uganda.