Mafuriko yahangaisha wakazi wengi wanaoishi kambini Tana Delta

  • | Citizen TV
    351 views

    Serikali inapania kununua kipande cha ardhi wanachoishi waathiriwa wa mafuriko Tana Delta kaunti ya Tana River. Katibu katika wizara ya usalama Raymond Omollo anasema hatua hiyo ndiyo suluhu ya maafa na athari za mafuriko kaunti ya Tana River na maeneo mengine. Na kama anavyoarifu Francis Mtalaki watu wanne wamefariki na zaidi ya watu 190,000 wakilazimika kutafuta makao mbadala katika kaunti hiyo pekee.