Skip to main content
Skip to main content

Magonjwa ya macho na koo yaongezeka kaunti ya Murang'a

  • | Citizen TV
    251 views
    Duration: 2:07
    Wataalamu wa afya katika kaunti ya murang’a wameelezea wasiwasi mkubwa kufuatia ongezeko la magonjwa ya macho na koo, huku wakionya kuwa ucheleweshaji wa utambuzi wa magonjwa ya macho unaweza kusababisha matatizo makubwa, ikiwemo upofu. Wakizungumza wakati wa kambi ya matibabu ya macho, masikio, pua na koo iliyofanyika katika chuo cha mafunzo anwai cha taifa cha michuki katika eneobunge la kangema, wataalamu wa afya walihusisha ongezeko hilo na kukaa muda mrefu chini ya miale ya jua, ambayo huharibu macho.