- 180 viewsDuration: 2:09Mahakama kuu ilimuondolea hatia ya ufisadi aliyekuwa gavana wa Samburu Moses Lenolkulal, kwenye uamuzi uliofutilia mbali kifungo cha miaka minane, kwenye kesi ufisadi wa shilingi milioni 83. Kwenye uamuzi wake, Jaji Benjamin Musyoki, alisema kuwa upande wa mashtaka ulishindwa kutoa ushahidi wa kutosha wa kuwa Lenolkulal alihusika na ubadhirifu wa fedha hizo, na kwamba aliitumia nafasi yake kama gavana kujifaidi.