Skip to main content
Skip to main content

Mahakama kuu yaagiza kusitishwa kwa mishahara ya washauri 21 wa Rais Ruto

  • | Citizen TV
    3,889 views
    Duration: 2:05
    Mahakama kuu nchini sasa imeagiza kusitishwa kwa mishahara ya washauri 21 wa Rais William Ruto, ikiamua kuwa uteuzi wao haukuwa halali. Jaji wa mahakama kuu Bahati Mwamuye akiitaka tume ya huduma za umma kusitisha mishahara yao huku akiagiza ukaguzi kufanywa katika muda wa miezi mitatu. Washauri wa Rais wanajumuisha mwana uchumi David Ndii, mshauri wa usalama Monica Juma, mwenzake wa katiba Makau Mutua na mshauri wa maswala ya wanawake Harriet Chiggai miongoni mwa wengine