- 1,064 viewsManusura wa ghasia za maandamano sasa wanamtaka Rais William Ruto kuwaomba msamaha wao moja kwa moja kutokana na dhuluma mikononi mwa maafisa wa serikali. Manusura hao wamekataa kile wanachokieleza kuwa msamaha wa rais ambao haujakamilika. Pia wanaitaka kamati iliyoshughulikia mipango ya fidia kuweka wazi orodha ya watu wanaotarajiwa kupokea fidia hizo.