Siku chache baada ya runinga ya citizen kuangazia masaibu ya shule ya kaburwet iliyoko eneo bunge la sirisia kaunti ya bungoma,wadau wa elimu, wakuu wa elimu na wazazi walizuru shule hiyo ili kutathmini hali.
Wakizungumza kwenye kikao Cha kupokea maoni ya umma, wazazi na viongozi hao wamesema hatua zifaazo zitachukuliwa iwapo marekibisho yaliyopendekezwa hayatatimizwa kwa wakati ufaao. Shule hiyo ilikuwa imeangaziwa kwa kukosa vyoo, madarasa ya kutosha na miundombinu mingine, kufuatia utepetevu wa usimamizi wa rasilimali na bodi ya shule.