Vikao vya bunge la seneti mashinani katika kaunti ya Busia vimetia nanga baada ya shughuli za wiki moja. Hata hivyo, kikao cha leo alasiri kilitatizika kutokana na idadi ndogo ya maseneta na ikabidi bunge liahirishe vikao vyake hadi saa kumi alasiri. Vikao vya bunge la seneti katika kaunti ya Busia viliwawezesha maseneta kutangamana na wakazi, kukagua miradi ya serikali ya kaunti pamoja na ile ya kitaifa pamoja na kutathmini matumizi ya fedha za umma za kaunti. Kamuche Menza na taarifa kwa kina.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive