Skip to main content
Skip to main content

Mashirika 390 ya kuajiri watu yanachunguzwa

  • | Citizen TV
    326 views
    Duration: 1:40
    Mashirika 390 ya kuwaajiri watu yanachunguzwa na serikali huku uchunguzi kuhusu mengine 15 ukiwa umekamilika na faili kuwasilishwa kwa mkurugenzi wa mashtaka ya umma. Ripoti ya jopokazi lililoteuliwa mwaka 2024 kuangazia malalamishi kuhusu shughuli za mashirika hayo imetolewa leo na waziri wa leba Alfred Mutua...Kati ya mashirika hayo 390, 106 yanahusisha kampuni za usafiri huku ikibainika kuwa baadhi ya watu binafsi na kampuni zinazowakilisha Wakenya hazijasajiliwa hapa nchini..