Wakulima na wafugaji kutoka kaunti ya Garissa sasa watakuwa wakipokea habari kuhusu utabiri wa hali ya hewa kwenye simu zao za rununu ili kujiandaa na kujiepusha na hasara zinazosababishwa na ukame na mafuriko.
Kwenye uzinduzi wa awamu ya pili ya mradi wa Wiser-Kenya mjini Garissa, Mratibu wa mradi huo amesema kwa ushirikiano na idara husika, pia wataangazia maeneo ya malisho kwa mifugo na lishe bora kwa watoto. Aidha mradi huu unalenga kuhamasisha wafugaji kuhusu umuhimu wa kuhifadhi chakula cha mifugo kwa matumizi wakati wa kiangazi.