- 6,224 viewsDuration: 2:59Mbunifu wa mavazi chipukizi nchini Tanzania Hassan Omar Mgaza ameiambia BBC wakati akianza shughuli zake za mitindo waliowengi walikuwa haelewi anachokifanya ikiwa ni pamoja na watu wake wa karibu kuhoji mavazi aliyokuwa kitengeneza yangevaliwa na nani? Hassan amejitambulisha kwa mitindo yake aliyoipa jina la mbele ya muda saa 72 na mpaka sasa amevalisha wasaanii na watu maarufu kadhaa nchini Tanzania na nje ya nchi huku akijinasibu soko lake kubwa ni nje ya nchi, karibuni alitwaa tuzo ya Swahili fashion week kama mtenezaji bora ya maudhui ya mitindo mtandaoni kwa mwaka 2025. Changamoto inayomkabili ni upatikanaji wa malighafi na fedha, Mwandishi wa BBC Eagan Salla alimtembelea na kutuandalia taarifa ifuatayo @gazaboe Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw