- 18,834 viewsDuration: 26sMeli iliyobeba lami iligonga meli ya kitalii iliyokuwa imetia nanga katika Mto Mississippi, karibu na bandari ya New Orleans nchini Marekani. Meli ya kitalii iitwayo American Heritage ilikuwa na watu 190 ndani yake wakati wa ajali hiyo, ambapo baadhi ya abiria waliokolewa huku wengine wakifanikiwa kujiokoa wenyewe. Baada ya kugongwa, meli hiyo ilipinduka ikiwa bandarini. Kwa mujibu wa maafisa wa usalama wa usafiri nchini Marekani, meli iliyosababisha ajali hiyo ilikuwa na hitilafu katika mfumo wa usukani. Hata hivyo, hakuna mtu aliyefariki katika ajali hiyo. #bbcswahili #ajalibaharini #marekani Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw