Skip to main content
Skip to main content

Mifupa ya binadamu imepatikana eneo la Karai, Kikuyu

  • | Citizen TV
    6,784 views
    Duration: 1:50
    Hali ya Wasiwasi imetanda katika Kijiji cha Karai, eneo bunge la Kikuyu, Kaunti ya Kiambu, baada ya mifupa inayokisiwa kuwa ya binadamu kupatikana katika uwanja wa Karai. Eneo hilo lina mabwawa na vyanzo vya maji, na hutumiwa na wakazi pamoja na watu kutoka maeneo jirani, hali inayozua wasiwasi mkubwa kuhusu usalama wao. Maafisa wa Polisi walifika katika eneo la tukio na kukusanya mifupa hiyo, ambayo imepelekwa katika maabara ya serikali kwa uchunguzi zaidi. Wakazi sasa wanatoa wito kwa serikali na mamlaka husika kuhakikisha mabwawa katika eneo hilo yanawekwa vizuizi, ili kuzuia visa vya watu kutumbukia humo