Skip to main content
Skip to main content

Msako wa wanafunzi Murang'a

  • | Citizen TV
    429 views
    Duration: 2:15
    Kufuatia agizo la Rais kuhusu wanafunzi wa Gredi ya 10 kuruhusiwa shuleni hata bila karo na sare rasmi, maafisa wa utawala katika Kaunti ya Murang’a wamesema watatembelea nyumba hadi nyumba kuwatafuta wanafunzi ambao bado hawajaripoti shuleni. Hatua hiyo inalenga kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanaopaswa kujiunga na shule za sekondari ya juu wamefika shuleni na kupata elimu. Wakizungumza wakati wa utoaji wa basari katika eneo bunge la Kangema, maafisa hao wamesema wanashirikiana kwa karibu na wazee wa vijiji pamoja na viongozi wa makanisa kuwapata wanafunzi ambao bado wako nyumbani.