- 20,390 viewsDuration: 2:56Mshukiwa wa tatu katika kesi ya mwanamke aliyemwagiwa asidi amekamatwa na kufikishwa kortini. Jared Olang Geng anadaiwa kupokea pesa kutoka kwa mshukiwa mkuu, Elvis Mara, huku mkewe akitarajiwa kuhojiwa baada ya uchunguzi kubaini kuwa simu yake ilitumika kupokea fedha kutoka kwa Mara. Mwathiriwa, Claire Ochieng, anaendelea na matibabu baada ya kupoteza uwezo wa kuona kwa zaidi ya wiki mbili kufuatia shambulio hilo.