- 1,974 viewsDuration: 3:09Waziri wa usalama Kipchumba Murkomen sasa anasema kuwa uvamizi katika kanisa la ACK Witima eneobunge la Othaya, ulisababishwa na uhasama wa kisiasa kati ya viongozi wa Nyeri. Murkomen aliyefika bunge la seneti Jumatano, alidai asasi za usalama Nyeri hazikufahamishwa kuhusu kuwepo kwa ibada iliyohudhuriwa na viongozi hao, na hivyo hawakutoa usalama. Na kama anavyoarifu Kamau Mwangi, Murkomen alikuwa na wakati mgumu kueleza seneti sababu za maafisa wa polisi kuendelea kuficha nyuso zao wanapofika kudhibiti hali.