- 18,431 viewsDuration: 3:16Waziri wa Usalama, Kipchumba Murkomen, na aliyekuwa Naibu Rais, Rigathi Gachagua, wamerushiana cheche za maneno baada ya Murkomen kuonya kuwa Gachagua ameibuka kuwa tishio kwa usalama wa taifa na kwamba atachukuliwa hatua za kisheria. Kwa upande wake, Gachagua anadai serikali inajaribu kuzima madai yake kuhusu ufisadi serikalini pamoja na kile anachodai ni njama mpya ya kunyakua kampuni ya maziwa ya New KCC. Mwanahabari wetu wa masuala ya kisiasa, Stephen Letoo, ana taarifa hiyo.