- 561 viewsDuration: 1:45Huduma za afya zilitatizika kwa muda katika zahanati ya lwandanyi eneo bunge la Sirisia kaunti ya Bungoma baada ya mvua iliyoandamana na upepo mkali kung’oa paa la zahanati hiyo usiku wa kuamkia leo . Kulingana na afisa msimamizi wa zahanati hiyo dakta Emmanuel Wepu, tukio hilo liliathiri pakubwa shughuli za kawaida hasa eneo linalohudumia wagonjwa wanaopokea matibabu kisha kurejea nyumbani . Wakazi wameitaka serikali ya kaunti kukarabati miundomsingi ya zahanati hiyo ili kukithi mahitaji ya idadi kubwa ya wagonjwa.