Mwakilishi wa kike katika kaunti ya Nyamira Jerusha Momanyi ameomba asasi za usalama kwa ushirikiano na jamii kuchukua hatua kali, dhidi ya washukiwa wa ubakaji wa watoto, kwani visa hivyo vinaongezeka katika kaunti hiyo.
Kisa cha punde zaidi kikiwa cha msichana mwenye umri wa miaka 5 kutoka eneo la Gesima aliyebakwa na kisha kuuwawa, huku mwili wake ukipatikana nyumbani kwa jirani yake. Akizungumza katika hafla ya ufadhili wa vyama vya ushirika katika eneo bunge la Mugirango Magharibi, Momanyi amesema visa hivyo vinachangiwa na uraibu wa dawa za kulevya na pombe haramu katika jamii.