Mwanablogu aliyefariki Kenya aliuawa na nani? Katika Dira ya Dunia TV

  • | BBC Swahili
    16,362 views
    Uchunguzi umeonyesha kwamba Albert Ojwang ambaye ni mwanablogu na mwalimu aliyefariki akiwa kuzuizini baada ya kukamatwa na polisi aliuawa. Matokeo ya uchunguzi huo uliofanywa na mpasuaji wa serikali Dkt. Benard Midia imetofautiana na taarifa za awali za polisi kwamba Ojwang alikuwa amejiumiza kwa kujipiga ukutani. Kulingana na uchunguzi wa leo, Ojwang mwenye umri wa miaka 31 alipata majeraha mabaya kichwani, kwenye shingo na majeraha kwenye mwili mzima. Hii ikionyesha kwamba kifo chake kilisababishwa na kujeruhiwa kimakusudi. Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw