- 774 viewsDuration: 5:39Familia moja kutoka kijiji cha Kodumo kaunti ya Homa Bay inaitaka serikali, kuwasaidia kumpata jamaa yao aliyekwama nchini Urusi. Richard Ouma, mwenye umri wa miaka thelathini alisafiri mwaka jana kama mtalii, na baadaye kuifahamisha familia yake kuwa amepata kazi katika kikosi cha vita cha Urusi. Hata hivyo, mawasiliano kati yao yalikatika na sasa hawajui hatma ya mpendwa wao.