Skip to main content
Skip to main content

Mwanamume adaiwa kumdunga kisu mkewe hadi kufa Kabare, Gichugu

  • | Citizen TV
    1,675 views
    Duration: 1:54
    Wingu la Simanzi limetanda katika mji Kabare eneo bunge la Gichugu Kaunti ya Kirinyaga baada ya mwanamke mwenye umri wa makamo kudungwa kisu hadi kufa na anayekisiwa kuwa mumewe kufuatia mzozo wa kinyumbani . Kulingana watu wa familia mzozo ulizuka wakati mke alimkataza mumewe kwa jina Daniel Muchira kuuza Ng'ombe wa pekee aliyekuwa akitegemea kama kitega Uchumi. inaarifiwa kuwa mwanaume huyo alimchoma kisu upande wa kushoto wa kifua, na kusababisha jeraha kubwa lililosababisha kifo chake na Kisha kutupa mwili wake kado ya Barabara . Wenyeji walimshika mshukiwa na kumpeleka katika kituo cha polisi cha kabare huku mwili wa marehemu ukipelekwa katika makafani ya Kerugoya Level Four.