MKASA WA MAPOROMOKO
Mwili mmoja umepatikana kutoka kwa vifusi vya jengo lililoporomoka katika mtaa wa South C jijini Nairobi, huku shughuli za uokoaji zikielekea hatua za mwisho. Waziri wa huduma za umma Geoffrey Ruku, akiandamana na viongozi kutoka kaunti za Marsabit na Nairobi amezihakikishia familia zilizoathiriwa kwamba serikali itagharamia mazishi, na gharama ya matibabu kwa majeruhi, huku uchunguzi kuhusu kiini cha ajali hiyo ukiendelea kukamilika. Huku hayo yaijiri, gavana wa Nairobi Jonhson Sakaja ametaka kurejeshwa kwa uwezo wa kuwafungulia mashtaka wastawishaji majengo wasiozingatia kanuni.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive