Skip to main content
Skip to main content

Mzozo wa ardhi umesababisha ghasia mtaani Mukuru

  • | Citizen TV
    5,248 views
    Duration: 1:38
    Ghasia zimeshuhudiwa katika eneo la Mukuru kwa Njenga, jijini Nairobi kufuatia ubomoaji wa majengo ili kutoa nafasi ya upanuzi wa barabara ya Catherine Ndereba Alipofika kutathmini hali Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja akijipata katikati ya vurugu hizo baina ya polisi na wakazi waliopinga zoezi hilo. Ubomoaji huo ulioanza mapema asubuhi ulisitishwa baada ya Gavana Sakaja kutoa amri ya kusimamishwa kwa shughuli hiyo. Sio mara ya kwanza vurugu za aina hii xinashuhudiwa. Mara kwa mara mamlaka ya barabara mijini KURA imekuwa ikijaribu kuondoa majengo yaliyo katika maeneo yaliyotengewa ujenzi wa barabara. Viongozi wakitaka utaratibu mwafaka ufuatwe kuhakikisha wakazi hawaathiriki.