- 776 viewsDuration: 2:18Wanakijiji wa Kinakomba kaunti ya Tana River wameandamana hadi katika ofisi za Kamishina wa kaunti hiyo kufuatia mzozo wa mipaka kati ya ardhi yao na kaunti jirani ya Garissa. Kulingana na wanakijiji hao, majirani wao wamekuwa wakiwatisha ilhali kuna mpaka uliowekwa na wakoloni na ambao unatambuliwa na serikali. Wakazi hao sasa wanaitaka tume huru ya uchaguzi na mipaka - IEBC - kuzuru eneo hilo na kutoa mwelekeo kabla ya hali kuwa mbaya zaidi.Kamishina wa kaunti hiyo alisisitiza kuwa sheria itafuatwa ili kubaini mpaka halali kati ya kaunti hizo mbili.