Naibu gavana wa Siaya William Oduol aliyebanduliwa ahojiwa

  • | Citizen TV
    1,278 views

    Naibu gavana wa Siaya aliyebanduliwa na bunge la kaunti hiyo William Oduol anasema kuwa anaadhibiwa kwa kufichua ufisadi katika kaunti hiyo. Oduol ambaye anahojiwa na kamati maalum ya seneti kuhusu ushahidi uliotolewa dhidi yake ambapo anatuhumiwa kwa ubadhifiru wa pesa za kaunti na kutumia ofisi yake visivyo miongoni mwa mashtaka mengine amesema kuwa kaunti hiyo na haswa gavana James Orengo ilikuwa inafuja pesa za kaunti. Kamati hiyo maalum itachunguza ushahidi dhidi yake kabla ya kuandaa ripoti kuhusu iwapo alibanduliwa ofisini kihalali au la.